Miongoni mwa mambo ambayo simu yako ya kisasa inaweza kuyafanya ni kukufahamisha ilipo
kuliko kompyuta yako ya mezani,kompyuta mpakato wakati mwingine hata tablet
ambavyo wakati mwingine ni vigumu kuwa navyo muda wote,simu za kisasa inaweza
kujumuisha eneo ilipo na data katika upatikanaji wa habari ama taarifa mbalimbali.
Kama ilivyo katika masuala mbalimbali ya teknolojia za
kidijitali uwezo huu wa simu una uzuri wake na ubaya wake.Watumiaji wa simu
wamekuwa wakijiuliza kuhusu masuala ya faragha hasa linapokuja suala la
kufahamu mtumiaji wa simu alipo katika usalama wake.
Pia watu wengine hawako makini nahawafahamu ni teknojia
gani ya kutambua mahali walipo na hasa kutokana na ukweli kwamba kuna
program tumishi nyingi ambazo huhitaji kuonesha mahali mtumiaji wa simu alipo.
1.GPS
Global Positioning Systeam ni mtambo wa satellite unaotambua
na kuelekeza maeneo mbalimbali hapa duniani.Mtambo huu unaoendeshwa na Kitengo
cha Ulinzi cha Serikali ya Marekani ulianza kutimiwa katika simu mwaka
1990.Teknolojia hii inafanyakazi masaa 24 kwa siku na inauhakika wa kutoa muda
halisi wa umbali Fulani,umbali wa mahali kwenda mahali pengine pamoja na kutoa
muda wa sehemu mbalimbali za dunia kwa wakati mmoja.
Teknolojia hii iliyopo katika simu za mikononi inaweza kutumika kuonyesha kifaa
kilipo,kitakapokwenda ama kilipo.
Baadhi ya serikali duniani zimetengeneza mifumo yake ya
GPS,japo haziingiliani na ule wa awali kwa kweli vinasaidia sana katika
kufahamu mahali ulipo.Warusi wanao unaitwa GLONASS na wachina wanayo ambayo
mwaka 2012 ilikuwa katika majaribio,Ulaya wanayo inaitwa Galileo na Japani
inaitwa Quasi-Zeneth.
Mwaka 2012 Watalaamu wa kuunda wa simu za mkononi walikuwa
katika mkakati wa kutengeneza processor ya simu ambayo itakuwa na uwezo wa kutumika
katika aina zote za mifumo hii ya kufahama mahali ulipo.
2. Cell ID
Pamoja na kuwepo kwa teknolojia ya GPS,Makampuni ya kutoa
huduma za simu kwa maana ya mitandao ya simu yanafahamu eneo na mahali simu
ilipo bila hata ya GPS,na walifahamu
hili hata kabla simu hazijawekewa technolojia hii
Makampuni yanafahamu ni simu ya aina gani mteja anaitumia na
umbali gani uliopo kati ya simu na simu nyingine kutokana na teknolojia iitwayo
Cell ID ama kitambulisho cha simu,ambapo miongoni mwa vitu vinavyosaidia
kufanyakazi kwa teknolojia hii ni minara ya simu.
3.WI-FI
Wi-Fi inaweza kufanya vyema kwa namna teknolojia ya Cell ID inavyofanyakazi ,japo si kwa uwezo
mkubwa sana kwa kuwa teknolojia ya Wi-Fi ina uwezo wa kufanya kazi katika eneo
dogo ambapo ni sawa na mita 100.
Teknolojia hii hutumia njia mbili ya kwanza ni ile
inayowezesha kuonesha kidokezo cha uwezo
wa kupokea masafa ya mawasiliano (RSSI) kwa kutumia masafa ya simu husika kwenye
mtandao wa Wi-Fi
Njia ya pili inayotumika katika Wi-Fi ni utumiaji wa alama
za vidole ambapo inaelezwa ni njema kwa mtumiaji wa ambaye anapenda kutembelea eneo fulani mara kwa mara
Alama hizo za vidole zinaweza kutambua mahali ulipo kwa umbali
wa mita chache.
4. Bluetooth
Naam utambuzi wa mahali unaweza kufahamika kwenye eneo
husika katika maduka yanayotumia kifaa
cha kufahamu na kutunza kumbumbu bei za bidhaa kiitwacho beacons ambacho
hutumia teknolojia ya Bluetooth,vifaa hivyo vinaweza kuwasiliana na simu ya
mkononi yenye teknolojia ya Bluetooth 4.0.
Hizi ni baadhi tu ya teknojia zilizopo katika simu za kisasa
ambazo zaweza kutumika kufahamu simu ilipo na hii inamaanisha kuwa simu
ikifahamika ilipo basi hata mtumiaji wa simu hiyo naye anajulikana alipo
kumbuka kadri teknolojia inavyotuweka
karibu unaweza kukimbia lakini huwezi kujificha
Chanzo: Maisha na Teknolojia
Chanzo: Maisha na Teknolojia
0 Comments
If you like this post be sure to leave a comment and share it with your friends. It will make my day!